https://lagradaonline.com/en/toyota-goodbye-electric-cars-new-engine/
Toyota says goodbye to electric cars – They are already preparing the new engine of the future
Toyota says goodbye to electric cars – They are already preparing the new engine of the future
Posted by Kennedytz at 2/10/2024 01:44:00 PM
https://x.com/mbezitznews?t=WI7lAn7eXAQa4B2mVF_ftQ&s=09
Posted by Kennedytz at 9/21/2023 07:26:00 AM
Posted by Kennedytz at 9/21/2023 07:24:00 AM
Zigor released a new modular bidirectional central inverter at the Genera trade show this week in Madrid, Spain. The Spain-based power electronics manufacturer said the three-phase system has an output of 2.68 MW, or 3.3 MVA, and a DC voltage ranging from 950 V to 1,500 V.
Posted by Kennedytz at 2/26/2023 09:04:00 AM
https://www.pv-magazine.com/2023/02/15/longi-releases-new-alkaline-electrolyzer/
Posted by Kennedytz at 2/17/2023 03:41:00 PM
Posted by Unknown at 9/03/2021 08:43:00 AM
Posted by Unknown at 10/26/2020 09:27:00 PM
NAKUMBUKA SAFARI YA MWANA HABARI KIJANA MARINI H MARINI ENGINEER.
Posted by Unknown at 4/02/2020 01:02:00 PM
Posted by Unknown at 3/23/2020 10:38:00 PM
Labels: Coronavirus disease (COVID-19)
CORONA NI IANGA LINGINE DUNIANI
Ebu tumuombe Baba Mwenyezi Mungu atusaidie kwa hili janga
Tuanze sasa kimya kidogo wapendwa..
Baba mwenyezi Mungu mwenye uwezo na nguvu kuliko yeyote..
Tunakuomba utusamehe yale yote tuliyoyafanya kwa kutokupendeza wewe...
Baba tusamehe na utupe nguvu ya kupambana na janga hili la corona linalotaka kuiangamiza duniani yote.
Baba kemea na uangamize corona kwa sauti ya neno moja tu, ili binadamu tujikinge na kusonge mbele na maisha yenye imani juu yako
Baba wape nguvu wanasayansi duniani kote ili wagundue kinga na dawa ya kuipoteza corona kusambaa duniani.
Baba wewe unajua nini kilichotokea mpaka corona kufika hapo.
Basi sisi wanao tunakuomba ili utuonyeshe matumaini kwetu. Tuweze kupambana na janga hili la corona ili dunia iendelee kama ulivyopanga.
Amina.
By
Kimaro
Posted by Unknown at 3/11/2020 08:31:00 PM
Labels: Corona Virus
https://www.forbes.com/sites/peterdetwiler/2019/12/11/inverters-the-unsung-hero-of-the-global-emerging-energy-economy/
Posted by Kennedytz at 12/12/2019 10:43:00 AM
https://www.pv-magazine.com/2019/11/27/new-methodology-for-assessing-value-of-pv-in-uncertain-markets/?utm_source=Bibblio&utm_campaign=Internal
Posted by Kennedytz at 12/12/2019 09:08:00 AM
https://www.pv-magazine.com/2019/12/11/neural-networks-improving-solar-power-forecasting/
Posted by Kennedytz at 12/12/2019 09:07:00 AM
Leo tarehe 21 sept 2019 Jumamosi ilikuwa siku ya kawaida kwangu Kama jumamosi nyingine.
Niliamka muda ambao uwa ni kawaida yangu siku zote.
Nilichukua mswaki nikaweka dawa ya mswaki ninyotomia kila siku aina ya whitening.
Uwa natoka nje ili nijifanyie mazoezi kidogo kupasha mwili moto na kuweka viungo sawa.
Niliondoka nyumbani saa mbili na dakika kadhaa nikawa nipo nje ya muda ambao sio rafiki
Nilipofika maeneo ya jirani na kazini nilienda kutafuta chapati moja ili niweke na ndizi nilizowekea na mke wangu kipenzi.
Kulikuwa hakuna chapati kisa anayezikaanga mkaa ulikuwa aujakolea moto..
Nikawasha gari kuelekea kazini.
Pembeni kulikuwa na vibanda vya mama lishe zaidi ya kimoja.
Katika kibanda kimojawapo walikuwepo wafanyakazi wenzangu wawili.
Ilinibidi nipaki gari karibu na walipopaki gari lao.
Nilipofika tukasalimiana nao uku nikivuta kiti na kukaa.
Wao walikuwa wakisubiri kifungua kinywa walicho kiagiza asubuhi hiyo.
Nikajeuka upande waliopo mama rishe na kuwauliza mtori upo.
Nilijibiwa na mmoja wao upo tele.
Nikawaambia lazima niuonje kwanza kabla ya kunywa.
Wakati nasubiria ili niuone uo mtori
Kumbe wenzangu nao walikuwa wanasubiri mtori pia.
Ukaletwa mtori wao bakuli mbili na chapati moja kwa kila bakuli.
Nami nikasema nipewe mtori kama ulioletwa kwa wenzangu.
Wakati bakuli yangu yenye mtori na chapati inafika mezani,
Kwa mbali Mzee mmoja alikuwa anakuja upande wetu akiwa mnyonge na upole kidogo.
Nikanyanyua kijiko na kuonja ule mtori kama unafikia kiwango cha kufanana na mtori.
Nilipouonja testi yake ilikuwa mtori ni mwepesi sana wakati kawaida ya mtori ndizi zinakuwa nyingi kuliko maji.
Nikauliza ni shilingi ngapi bakuli moja na chapati moja.
Kwa mbali mama lishe akanijibu ni elfu moja na mia mbili hivi.
Wakati huo yule babu alikuwa amefika karibu yetu
Nilipomuona tu na onyonge wake, basi kama kawaida yangu huruma umetawala fikra zangu
Mungu akaniambia msaidie huyo mzee hili asubuhi iwe ya furaha kwake pia.
Bila kusita nikajeuka kwa yule mzee na kumwambia karibu upate mtori huku unikitumia jina babu.
Yule Mzee akacheka kwanza na kusimama pale alipo kwa sekunde chache.
Mzee akajeuka upande wetu na kuelekea katika meza iliyo karibu yake.
Alivuta kiti na kukaa kusubiria aletewe mtori na mama lishe.
Ndipo nilpowajeukia mama lishe na kuwasisitiza walete mtori kwa Mzee.
Najua unashangaa kuona natoa hisani ya mtori kwa huyo mzee na nimepata wapi nguvu kama hiyo.
Nguvu ya Upendo kwa binadamu kusaidiana wenyewe kwa wenyewe inatokana na upendo wa Yesu kwetu.
Yesu litenda maajabu na kutufundisha mengi yenye hekima ili iwe mifano na mafunzo kwetu daima milele.
Katika safari zake nyakati hizo watu walikuwa wakimfuata ili wasikilize mafundisho yake.
Ndipo siku moja walipokusanyika watu wengi na kukosekana chakula cha kuwapa
Ndipo
Yesu alichukua vipande mikate na Samaki ili wote waliofika katika mkusanyiko wapate chakula.
Nguvu ya kuwalisha umati wa watu alionyesha Yesu ni nguvu ya Mungu baba kwetu ili sisi kupata msamaha wa dhambi zetu.
Nikatoa noti ya elfu kumi na kumpa mama lishe.
Ili iwe malipo ya mtori kwa sisi watatu na yule babu.
Mama lishe akanipa chenji yangu nami nikaipokea na kuiweka mfukoni tayari kwa kuondoka eneo hilo.
Sisi tulielekea kazini kama kawaida yetu Ila muda huo tukawa tumechelewa kidogo.
Tulianza kazi kama kawaida, tulishambulia kazi zilizokuwa zimebaki jana yake na kuzimaliza zote.
Tukaendelea kufanya kazi zote za siku hiyo ya jumamosi.
Ilipokaribia saa tano nilienda kuchukua diary yangu ili nienda katika kikao cha kila siku.
Tulipotoka katika kikaoni tukaunganisha kikao kingine cha pili.
Kawaida ya kila jumamosi panakuwa vikao viwili tofauti.
Kumbuka muda unasonga mbele bila kumngojea yeyote hapa duniani.
Ilipofika saa saba ikawa nimemaliza majukumu yangu yote ya siku hiyo.
Nilianza kijitayalisha kurudi nyumbani kwa mapumziko ya jummosi.
Nikawa napanga nikapate chakula cha mchana aina ya ugali na makange kule ninapoenda kula kila jumamosi.
Unajua ugali ukiwa wa moto na mboga ni rosti ya nyama yenye pilipili kwa mbali iliyochaganyika na mbogamboga na matunda ni Burudani sana.
Mara nikakumbuka kuwa watoto wanaitaji vitabu kwa ajili ya shule na leo nina nafasi ya kwenda kuwatafutia.
Nikachukua simu yangu nakumpigia mama wawili mke wangu ili afanye mambo mawili.
1. Aje kuchukua begi langu la ofisni hapo barabarani, kwani sitapitia nyumbani kwa wakati huo.
2. Anitumie picha za vitabu vinavyotakiwa katika WhatsApp yangu.
Nilitoka maeneo kazini na usafiri wangu mpaka kituo cha mafuta kilicho karibu.
Nilienda hapo hili kuongeza mafuta kidogo na kuangalia tairi za gari kama zina upepo Wa kutosha, kwa sababu ni siku nyingi sijaongeza upepo katka tairi zote.
Nilifanikiwa kuongeza mafuta tu Ila upepo haikuwezekana kwa sababu kulikuwa na foleni nami nikaona natachelewa kufika kariakoo.
Ilibidi niondoke hapo na kuendelea na safari yangu ya Kariakoo.
Nilipofika karibu na nyumbani nilimkuta mama wawili njiani akinisubiri, nilimpa begi langu nami nikaendelea na safari yangu ya Kariakoo.
Nilipofika maeneo ya tangibovu ilinibidi niingie kituo cha mafuta. Ili niongeze upepo tairi zote.
Zoezi ilo lilifanikiwa hapo katika kituo cha mafuta cha oil com
Safari ilianza hapo mpaka taa za kuongoza magari kona ya kuelekea kawe eneo la lugalo kambi ya jeshi.
Kituo cha pili kikawa taa za kuwavusha wanafunzi maeneo ya makongo.
Hapa kuna taa kwa ajili ya wanaotembea kwa mguu kuvuka njia nne bila shida.
Mtu yeyeto akiwa upande wowote anabonyeza kitufe na taa nyekundu inafuata ili nagari yasemame kuwapa watu fulsa ya kuvuka bila matatizo.
Kituo cha tatu kikawa taa za kuongoza magari njia nne mwenge kushoto kuelekea kiwanda cha soda cha cocacola na upande wa kulia ni kwenda mlimani city.
Tunapotoka hapo tukanyosha moja kwa moja
Kituo kilichofuata ni taa za kuongoza magari BamagaTBC. kona ya kwenda sinza na upande wa kushoto studio za TBC.
Tulipotoka TBC tukafika taa za kuongaza magari zamani palikuwa. panaitwa maji mchafu au sasa sayansi TTCL hapo taa zilikuwa kijani tukapita bila kusimama.
Unajua bahati uonekana mapema asubuhi nilipofika moroko kwenye njia panda kushoto ni kuelekea msasani na kulia kwake ni barabara ya kinondoni.
Mimi nikiwa natokea Mwenge naelekea mjini hapo tukanyosha moja kwa moja.
Kwa sababu taa za kutongoza magari zilikuwa kijani hakuna kusimama hapo moroko traffic light.
Tulipofika taa za Namanga kona ya kwenda msasani tulipunguza mwendo kidogo na kusimama hapo kwa sekunde chache.
Taa zilipowaka kijani tukaenda taratibu mpaka taa za kona ya kwenda kanisa katoriki saint peter. kwa bahati nzuri taa zilikuwa kijani.
Nilipita hapo kwa mwendo wa kawaida Kama ni dereva utanielewa tu.
Tulipofika mataa ya njia panda ya kwenda Kinondoni palikuwa na askari wa usalama barabarani yeye alikuwa akiyaongoza magari yaliyokuwa yanatoka upande wetu na upande wa mjini.
Hapo spidi ilikuwa ya wastani hivi kwa sababu magari yalikuwa karibu karibu.
Unajua macho yanapenda kuangali bahari
Eneo hilo upande wa mkono wa kushoto ni bahari .
Basi upande wa kushoto ukishapita taa za kuongoza magari kabla ya daraja la salender bridge kuna ujenzi unaendelea katikati ya bahari.
Unajua serekali ya awamu hii wanafanya kazi kweli kweli.
Mungu awape nguvu ya kutoangalia nyuma Ili wasonge mbele kuendeleza maendeleo nchi yetu yawe ya kimataifa na mfano kwa wengine.
Kuna kazi inaendelea ya ujenzi wa daraja kubwa la kisasa linalokatiza baharini lenye urefu wa kutosha linaloigharimu serekari mabilioni ya pesa.
Ni changamoto ya maendeleo katika karne hizi za sayansi na kiteknolojia kama zawadi kwa watanzania kwani daraja la kwanza lilijengwa mwaka 1929 na kutumika kwa takribani miaka 51.
Ndipo mwaka 1980 serekali wakajenga daraja la pili lenye heshima yake kwa wakati huo.
Mnamo mwaka 2014 waziri wa ujenzi wakati huo Mweshimiwa Mgufuli alitangaza serekali inategemea kujenga daraja kubwa la kisasa maeneo ya salander bridge
Umeonaaa pale penye maendeleo ya kweli lazima utajikuta unatoa maelezo yasio na mwisho.
Mara kushtuka mataa ya salander bridges.
Kushangaa kote ningepitiwa na kunyosha kwenda katikati ya jiji.
Hapo tulisimama kwa dakika chache kwa sababu aliyekuwa akiongoza nagari ni askari wa usalama barabarani.
Ikanibidi nikae upande wa kulia barabara ya Alli Hassani mwinyi ili niweze kuingia barabara united nation.
Dakika chache tukawa tumeingia Barbara ya umoja wa mataifa.
Njia ilikuwa nzuri kwangu , najua unasema kwanini.
Gari ya kwanza ilikuwa ya kwangu kwa hiyo nilikanyaga mafuta ili niwe wa kwanza kufika taa za fire zimamoto..
Katika taa zimamoto njia panda kushoto unaenda katikati ya jiji, kulia unaenda Magomeni.
Kwa wakati huo taa zikawa kijani hapo utata usipokuwa mjanja utabaki katikati.
Kwani taa za hapo zipo ruksa kwa wote .
Tukapita wote.
Mimi ikabidi niende mpaka maeneo ya kariakoo upandwe wa shule ya uhuru ili niweze kupata parking ya uwakika.
Nilipata sehemu ya kupaki Gari ambopo uwa napaki kila niendapo Kariakoo.
Kama nilivyokupasha hapo nyuma nia yangu ya kuja huku ni kutafuta vitabu vya watoto.
Hiyo siku ilikuwa ni siku yangu ya kutembea nilitembea kupita kiasi.
Hapa nawasubiria google watoe timeline yangu ya mwezi wa tisa ili nione mzunguko wangu ulikuwaje.
Wakati Natoka Kariakoo sokoni kuelekea mzunguko wa msmbazi.
Nikiwa maeneo ya jengo DDC karikooo gafla kwa mbele mama mmoja aliyekuwa amembeba mtoto mdogo alianguka huku mtoto akiwa mikononi mwake.
Alipokuwa anatembea hapo bahati mbaya akalanyaga banda la ndizi na kuteleza akaanguka chini.
huyo mama alikuwa amefuatana na watoto wake wa kiume wawili si wakubwa sana Ila ni Kati ya miaka kumi na mwingine nane hivi.
Yule kijana mkubwa akakimbilia mama Yake na kumbeba yule mtoto mdogo ambaye wakati uo alikuwa akilia kwa sauti kubwa.
Watu waliokuwapo eneo hilo hakuna hata mmoja aliyejaribu kumpa msaada yule mama kwa muda wote.
Mungu akanipa nguvu nilikimbilia pale na kupata nguvu ya kuwasogeza watu waliomzunguka yule mama wakimshangaa bila kutoa msaada wowote.
Huwezi amini yule mama alikuwa hawezi tembea ananyonga mguu kwa maumivu makali na kulia kama mtoto mdogo.
Mungu akanimbia wewe ni mwanajeshi kwa wakati huu onesha nguvu yangu kupitua kwako.
Basi niliinama na kumuambia yule mama nipo hapa kwa ajili yako sima nikumbatie mimi begani ili nikupeleke pembeni kwani hapo upo njiani na watu ni wengi watakukanyaga.
Mungu ni wa ajabu nilipata nguvu nikamtoa yule mama pale njiani na kumuweka pembeni ya jengo la DDC karibu na duka moja lililokuwa wazi.
Nikamuliza yule mama nini tufanye au tumpeleke hospital.
Kabla ya ajato jibu swali lingine kwa yule mama
Unaishi wapi hapa Dad es salaam.
Yule mama akajibu mtoni kijichi
Daa ni mbali toka hapa tulipo Kariakoo.
Bila kupoteza muda pembeni yetu wapo madereva wa tax...
Nikamfuata mmojo wa wale madereva
Nilipomueleza kuna mgonjwa anaitaji msaada kupelekwa hospital iliyo karibu na anapokaa mtoni.
Yule dereva akaondoka bila jibu , alipokuwa akiondoka akaenda kuongea na mwenzake .
Naye alipokuja akaja na vikwazo vya kumwacha njiani kwani hiyo ni kesi.
Akili yangu ikakumbuka bajaji ndipo nilipouliza zipo wapi! walio karibu yangu wakainua kichwa kuangalia upande wa pili wa barabara ya msimbazi.
Ndipo nilipoanza kukimbia kuelekea sehemu bajaj zilipopaki.
Nilipofika hapo nikaanza kupatana bei ya kutoka kariakoo mpaka mtoni kijichi.
Ndipo dereva wa bajaji akakubali kwa elfu kumi na tano.
Nakumbuka nilimuambia nifuate huku.
Mimi nikatoka mbio kuelekea kwa mgonjwa wetu
Bajaj ilipfika nikamuomba mama mmoja aliyekuwepo katika eneo hilo kumnyanyua ili tupeleke katika bajaji.
Kawaida msimbazi eneo la DDC uwa na watu wengi kwa nyakati za mchana tens siku za jumamosi.
Ilibidi nipangue njia kwa sauti kubwa Sogea sogea kama mimi mwanajeshi sauti yangu ilisikika kaa pembeni pisha pisha sogea wewe vipi kaa pembeni.
Na mungu ni mwenye nguvu watu wanasogea bila ubishi mpaka na wengine mpaka wajeuke nyuma wakimuoa yule mgonjwa wanapisha pembeni.
Yule mama kwa mbali niliskia akisema asante Sana Mungu atakubaliki
Basi vitabu venyewe sikuvipata Ikabaki kurudi nyumbani.
Kama una maoni yoyote
kimarokenny@gmail.com au
+255769922003
Mwisho.
Kennedy Kimaro
Posted by Kennedytz at 9/21/2019 08:09:00 PM
Sipati picha kwa majonzi yaliyomo ndani ya moyo wangu kutokana na ajali, iliyosababisha vifo vya watu saba miongoni mwao wafanyakazi watano wa Azam Media.
Najaribu kuvuta picha kwa vijana mafundi wachapakazi hodari jinsi ndoto zao na mipango yao katika taasisi ya habari chini ya movuli Azam Media Group.
Maisha ni sawa na universe ilivyo na umbo kubwa na umbali husiogawanyika na namba yeyote.
Unaanza mipango yako vizuri bila woga lakini huwezi tazama mbele kuna nini.
Nikijaribu Najaribu kuinua macho yangu juu na kupeleka fikra zangu za ujana kwa vijana wenzangu Azam Media.
Basi nabaki katikati ya fikra na kunyamaza kimya huku simanzi za machozi zikinijia kwa mbali.
Maswali mengi yamejikita katika fikra za ubongo wangu kutokana na tukio hilo la ajali.
Mawazo mengi yanakuja mbele yangu, lakini sipati picha katika fikra zangu, nini kilichotokea na kupelekea kubaki kimya.
Sisi ni binadamu na yale yote yaliyotokea tunayaona sisi tuliobaki hapa duniani.
Lakini vijana hawa.
1. Salim J Mhando
2. Silvanus W Kassong
3. Charles Wandwi
4. Florence B Ndibalema
5. Said H Hassan
Tuwawashia mishumaa ya maombolezi kwa wote watano
Safari yao ya hapa duniani ndio imefika mwisho.
Majonzi na maumivu ya simanzi zinabaki kwetu tulio hapa duniani.
Nashindwa kuendelea kuandika chochote zaidi ya kuwaombea wale wote waliofariki.
Nanyamaza kimya na kuangalia dunia inavyo songa mbele kwa spidi.
Na
Kennedy Kimaro.
Posted by Kennedytz at 7/09/2019 09:22:00 PM
Watu wenye tabia za ubaguzi na umimi kama hawa ni hatari sana.
Dunia imekuwa kama kijiji katika karne hii kutokana na ushirikiano wa kisayansi na teknolojia.
Inapelekea watu kuingia kona zote za dunia ili wawekeze na kutafuta kazi za kufanya kupata kipato na kuongeza kasi ya maendeleo na uchumi kupata nguvu ya kusonga mbele.
Hapo inapelekea binadamu kujichanganya katika jamii mbali mbali na kusababisha wakenya kuweza kuchumbia au kuoa mtanzania au mganda, vivyo hivyo kwa waganda na watanzania na dunia nzima.
Tena sio east Afrika tu, watu wanaoana toka sehenu mbalimbali hapa duniani mifano middle east, Europe, Asia, Russia, America
Ukianza kuwabagua wengine na kujifanya nyie ndie mwenye Fulsa ya kustahili kupata kitu au haki fulani, hiyo tabia ni hatari sana katika kizazi hiki cha sayansi na teknolojia.
Chuki za namna hii ni sawa kupanda mizizi ya magugu maji katika maisha ya binadamu.
Ukiwa na tabia ya chuki na ubaguzi kama hii ni hatari sana, haiwezi ishia hapo. itaendelea kwa vizazi na vizazi.
Baadaye uacha picha yenye mfano mbaya kwa watoto wetu.
Tabia kama hizi zikijitokeza lazima zikemewe mara moja.
Tabia kama hizi zinajenga uchochezi utaokufanya kesho kuanza kuwabagua hata ndugu unawaona sio wa karibu yako..
Siasa za namna ni hatari sana katika jamii zetu na kizazi cha vijana wa sasa.
Tumpe sifa Nyerere kwa kutuepusha na mambo kama hayo.
Sisi wabongo hapa kazi tu.. njoo na fedha zako.
Wekeza kwetu ili uongeze ajila kwa watanzania.
Tunajikita katika sera za kuongeza viwanda katika nchi yetu bila ubaguzi kwa raia yeyote kutoka mahali popote.
Kinachotakiwa uje na sifa za kuwekeza ili uchumi wetu upande juu.
Hiyo ndio Tanzania ya sasa yenye picha ya maendeleo kwa wote. 😄🥺👆
Wako @Kimaro.
Posted by Kennedytz at 6/26/2019 06:01:00 PM
JAMANI MAISHA NI HADITHI YENYE STORI INAYOANZA BILA WEWE KUJUA NA INAISHA BILA WEWE KUJUA.
KWANZA JIULIZE WEWE UPO UPANDE GANI WA HADITHI HII KATIKA MAISHA YAKO KILA SIKU.
PILI JIULIZE KUNA USHAWISHI WOWOTE ULIFANYIKA ILI UZALIWE KATIKA FAMILIA ULIYOPO SASA.
JIBU LITAKUWA HAPANA ILA MUNGU NDIYE ANAYEPANGA YOTE YAFANYIKE.
MUNGU ALI MUUMBA MTU AKASEMA NA TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU. KWA SURA YETU.
WAKATAWALE SAMAKI WA BAHARINI NA NDEGE WA ANGANI NA WANYAMA NA NCHI YOTE PIA.
HAPO NDIPO HADITHI NZURI YA MAISHA ILIPOANZA NA KUSABABISHA KIZAZI KU- TAWANYIKA DUNIANI KOTE.
HAPO MAISHA YAKAANZA NA KUKAWA NA WATU WENYE MUONEKANO TOFAUTI KUTOKA NA MAENEO WALIYOKUWA.
MAISHA YAKAWA YAPO YAKASABABISHA WATU KUWEPO KWA WAKATI NA YENYEWE YANAENDELEA TU DUNIANI.
MIMI NIPO NA NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIPA NAFASI MPAKA SASA.
UNAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KUKUPA NAFASI YA KUENDELEA KUWEPO MPAKA SASA.
SASA TUTAZAME NINI KILICHONISABABISHA KUYAANDIKA HAYA MACHACHE KWAKO.
MNAMO MWAKA 1996 MAMA MMOJA TOKA MKOANI IRINGA WILAYA YA MAKETE ALIBEBA MIMBA KWA MIEZI TISA KAMA KAWAIDA YA WANAWAKE.
ILIPOFIKA MUDA WA KUJIFUNGUA KAMA WAZAZI WENGINE.
NDIPO ALIKWENDA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI IKONDA MKOANI IRINGA ILI KUPATA HUDUMA ZA UZAZI..
ALIJIFUNGUA WATOTO MAPACHA WAWILI WALIOUNGANA MWILI.
HADITHI YA WATOTO WAWILI WALIOUNGANA ILICHOMOKA HAPO NA WATOTO KUPEWA MAJINA YA MARIA NA CONSOLATA MNANO MWAKA 1996.
KANISA LILIWACHUKUA MARA MOJA MARIA NA CONSOLATA WAKAWA CHINI YA SHIRIKA LA KIKRISTO.
CHA KUPENDEZA KWA AKINA MARIA NA CONSOLATA WALIJIONA WAPO SAWA NA WATU WENGINE.
MAISHA YAO YA KUKUBALI MATOKEO ULEMAVU WAO MOYONI NDIO UWEZO NAFSI YA IMANI WALIYOPEWA NA MWEYEZI MUNGU.
MSIMAMO WA KUENDELEA NA MICHAKATO KUENDELEA KUJIKITA KATIKA VITU VYA KIDUNIA.
IJAPOKUWA WAO NI WALEMAVU NI FUNDISHO KWETU LISILOKUWA NA MFANO.
MUNGU ALIWAPA MARIA NA CONSOLATA HEKIMA NA UWEZO WA KUWA WALIMU NA KUTUACHIA MFANO KWETU KUTOKANA NA MATENDO YAO.
INGAWA LEO HAWAPO TENA DUNIANI LAKINI BADO TUTAWAKUMBUKA.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA
WAPUMZIKA KWA AMANI.
KENNEDY MARO
Posted by Kennedytz at 6/06/2018 12:07:00 PM
Mara nyingi napenda kusikiliza maubiri ya neno la Mungu toka kwa wachungaji tofauti hapa duniani.
Lakini napenda mchungaji anayetumia maandiko ya biblia kama nguzo yake ya kuubiri amani.
Mungu ambariki na kuwaonyesha njia watumishi wake walio wengi kulisambaza nene lake.
Ndio maana roho mtakatifu aligawa nguvu za lugha tofauti ili neno lisambae duniani kote.
Kazi ya kulisambaza neno la Mungu pande zote duniani ni kazi ya kila mmoja wetu.
Kuna kitu kimoja ambacho kinanionya kutojaji imani ya dini ya binadamu mwingine yeyote, kwa sababu yeye au mimi tuna utashi wa kuwa upande wa imani wowote bila kulazimishwa na mtu yeyote.
Imani ni njia ya binadamu kujenga mahusiano kati yake na Mungu.
Imani ndio njia yenye nafasi ya matumaini kwa kila mtu kufanya mahamuzi ya kujijenga katika mahusiano yenye ushawishi wa nafsi yake na Mungu.
Tulipewa nafsi yenye imani ili kulitangaza neno lake Mungu kutoka katika masoma au mafundisho yaliyopo katika vitabu vitakatifu katika biblia.
Vitabu vitakatifu vinavyotumika kufundisha yale yaliyo na hekima ili kutufungulia upendo wa kweli toka kwa Yesu kristo.
Upendo wa mafundisho ya Yesu kristo ni njia yenye mafunzo yake kwa upeo na busara na amani.
Yesu alikuja na kutufundisha yale yaliyo mema ili kutufungulia njia ya faraja katika safari ngumu hapa duniani.
Mafundisho yake yote yalikemea mabaya na kukataa kurudia maneno mabaya.
Mungu alikemea matendo mabaya kwa kutufundisha kutenda yaliyo mema.
Mfano kitabu cha waamuzi mlango wa 13 kinatufundisha hivi...
MLANGO 13
1 Wana wa Israeli wakafanya tena yaliyo mabaya mbele za macho ya Bwana, Bwana akawatia katika mikono ya Wafilisti, muda wa miaka arobaini.
2 Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.
3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.
4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;
5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.
6 Ndipo yule mwanamke akaenda akamwambia mume wake, akisema, Mtu wa Mungu alinijia, na uso wake ulikuwa kama uso wa malaika wa Mungu, wa kutisha sana; nami sikumwuliza, Umetoka wapi? Wala hakuniambia jina lake;
7 lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.
8 Ndipo huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo kumfanyia huyo mtoto atakayezaliwa.
9 Mungu akasikiza sauti ya Manoa; naye malaika wa Mungu akamwendea yule mwanamke tena alipokuwa anaketi shambani; lakini mumewe, Manoa, hakuwapo pamoja naye.
10 Basi huyo mwanamke akaenda haraka, akapiga mbio, na kumwambia mumewe, akisema, Tazama, huyo mtu amenitokea, huyo aliyenijilia siku ile.
11 Basi Manoa akainuka, akamwandama mkewe, na kumfikilia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Naam, ni mimi.
12 Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia, je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini?
13 Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, Katika hayo yote niliyomwambia huyo mwanamke na ajihadhari.
14 Asile kitu cho chote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu cho chote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze.
15 Kisha Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana, Nakuomba, tukuzuie, ili tupate kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako.
16 Lakini malaika wa Bwana akamwambia Manoa, Ujapokuwa wanizuia, sitakula katika mkate wako; na kwamba wataka kufanya tayari sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsongezea Bwana. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa Bwana.
17 Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana, Jina lako ni nani, ili kwamba hapo hayo maneno yako yatakapotimia nipate kukutukuza?
18 Huyo malaika wa Bwana akamwambia, Kwani wewe kuniuliza jina langu, kwa kuwa jina hilo ni la ajabu?
19 Basi Manoa akamtwaa yule mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, akamtolea Bwana hapo juu ya mwamba; huyo malaika akatenda la ajabu; Manoa na mkewe wakaangalia.
20 Kwa maana, ikawa, mara huo mwali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa Bwana akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu; nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakainama kifudifudi.
21 Lakini malaika wa Bwana hakumtokea Manoa tena, wala mkewe. Ndipo Manoa alipojua ya kwamba ndiye malaika wa Bwana.
22 Manoa akamwambia mkewe, Hakika yetu tutakufa sisi, kwa sababu tumemwona Mungu.
23 Lakini mkewe akamwambia, Kama Bwana angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonyesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu.
24 Basi yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni
Posted by Kennedytz at 5/27/2018 08:27:00 PM
UPENDO UNAOTOKA KWA MTU NI TABIA YA NAFASI KATIKATI MOYO WAKE.
UPENDO SIYO KITU CHA KULAZIMISHA. UPENDO NI IMANI ILIYO YA KWELI KATI YAKO NA MUNGU.
Posted by Kennedytz at 4/06/2018 11:50:00 AM
MLANGO 20
1 Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.
2 Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu
3 Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi;
4 na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.
5 Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile.
6 Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
7 Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu
8 Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza.
9 Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari.
10 Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.
11 Basi wakiisha kuipokea, wakamnung'unikia mwenye nyumba,
12 wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.
13 Naye akamjibu mmoja wao,
akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?
14 Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.
15 Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?
16 Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho
Posted by Kennedytz at 2/18/2018 04:57:00 PM
Maisha ya leo ni tafu Kwa vijana wa leo.
Najua unanishanga kunisikia nikisema jinsi nilivonena hapo juu.
Wewe Mtanzania tazama jinsi ulivyo kama wewe unavyo starehe kwa kujikimu na kutatua ukata wa maisha hapa ndani ya jiji la Makonda.
Najaribu kuvuta picha na kuangalia jinsi ya maisha yetu yalivyogawanyika katika tabaka mbalimbali zenye tofauti ya maslahi.
Kabla ya kujikita katika gumzo na stori iliyopita mbele ya macho yangu na kuniweka katika tabaka la mawazo.
Najaribu kukuvuta mawazo yangu, ili nawe ufanye utafiti wenye njia iliyo na mistari sambamba yenye kukuonesha miangaiko wanayopitia wasio na uwezo katika jiji la Makonda.
Najua mawazo yako yatakimbilia kwa maskini walio wengi wanajulikana kama ombaomba wa mitaani.
Funga na fungua macho yako katika mtazamo wenye fikra zenye wigo mpana.
Tazama kwa umakini mkubwa kuwa jamii yenye umaskini si ombaomba tu.
Kuna watoto wengi wanaishi katika mazingira mgumu duniani kote.
Kuna watoto wanaofanyishwa kazi ngumu majumbani na maeneo yenye vita za wenyewe kwa wenyewe.
Tupia jicho lako utazame watoto wanaozaliwa na kutopewa malezi na wazazi wao na kupelekea kuwa watoto wa mitaani.
Jaribu kuvuta picha na kuangalia jinsi ya familia maskini katika maisha ya kila siku jinsi wanayopata taabu za chakula nguo na mahitaji yao kwa ujumla.
Tazama maisha yako na uleule upande wa pili tupia jicho kwa familia maskini.
Jitazame chai yako ya asubuhi gharama yake ni shilingi ngapi!
Jitazame chakula chako cha mchana Chips kuku na vingine vya thamani bei yake ni kiasi gani.
Tazama wangapi wanakwenda kunachangia mchango angalau kidogo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Jaribu kuelewa ni nani mchango wako katika familia zisizojiweza katika maisha yao kila siku.
Ebu twende na mimi bega kwa bega upate kujua kipi ninacho.
Jumapili nikiwa katika gari eneo la Mataa ya kuelekea Msasani, wakati huo taa nyekundu zimewaka upande wetu.
Magari yanayotokea mjini kuelekea msasani yalikuwa yanapita, upande mwingine kuna mistari ya pundamilia ya watembea kwa miguu kukatiza barabara.
Kukawa na kijana mmoja ukimtizama utamuona ni wa kawaida tu.
Cha ajabu uyo kijana mawazo yake hayakuwepo pale alipo.
Basi yule kijana akawa anavuka barabara bila ya kujali kuna gari linakuja au vipi?
Kufumba na kufungua gafla gari ikafungwa breki miguuni kwa yule kijana.
Ikabidi arudi nyuma ili gari lipite, tulipo mwambia kulikoni ndugu yetu huna macho.
Yule kijana akajibu ni maisha ndio yanafanya hivi.
Hapa tangu asubuhi sijaonja chochote kinywani.
Mchana umeshapita naungalia hivi hivi.
Kingine kinachonitesa hapa kwamba sijui nitafika vipi Mbagala wakati nipo msasani na sijui nipo katika dunia hii au vipi.
Sina hata sentano hapa mfukoni, ni taabu na shida katika maisha yangu.
Nakumbuka mimi ndio gari ya kwanza mbele, niliyaona yote yakitokea
Basi haraka nikatoa shilingi elfu moja na kumpa yule kijana.
Sikutegemea kitu alichokuwa akifanya yule kijana.
Alipiga magoti na kunishukuru huku machozi yakimtoka na akionyesha mikono juu kumshukuru Mungu.
Wakati huo taa za barabarani zinawaka kijani nasi tuliondoka.
Lakini njiani nikawa na uchungu wa moyo
Itaendelea
Wako
Kennedy Kimaro
Posted by Kennedytz at 7/24/2017 07:32:00 PM
Ebu tubige stori fupi kidogo ya maisha ya vijana wa sasa.
Kila asubuhi baada ya kujiweka sawa kwa safari ya kibaruani.
Nilipata chai ya asubuhi kama kawaida. Nikabeba simu zangu mbili na funguo za gari yangu.
Nilitoka nje ya nyumba yangu kuelekea kwenye gari yangu.
Mama watoto na watoto wakaja kunifungulia Gqeti kama kawaida yao.
Wakati ninarudi nyuma na gari, uku niki seti redio station moja ili kupata taarifa za kila siku.
Kukawa na watangazaji katika kipindi kimoja cha asubuhi wakitafakari yaliyondikwa kwenye magazeti ya siku hiyo.
Kikubwa kilikuwa ni mwanasheria ambaye ni mwana siasa wakati alipogoma kutoka ndani ya mahakama kuepushwa kukamatwa na polisi.
Wakati huo mtangazaji mmoja a akitoa stori ya kibaka au mwizi sugu aliyekimbizwa mitaa ya kawe na kufananisha suala la yule mwanasiasa
Stori ilianza hivi, yule mwizi alipokuwa akakimbizwa na raia wenye uchungu wa kuibiwa kila mara nyakati za usiku wa manane.
Wakawa wanamkimbiza yule mwizi kimya kimya ili wamshikishe nidhamu ya kutorudia tabia ya wizi.
Yule mwizi kwa mwendo kasi akakatiza karibu na kituo cha polisi cha kawe.
Alipoangalia kwa mbele akawaona askari wamesimama eneo la mapokezi.
Moyoni akasema liwalo na liwe maisha ni matamu, nikipoteza muda nitapata kichapo cha nguvu na kupoteza maisha hapa.
Basi yule mwizi akaongeza mwendo kuelekea upande walipo askari polisi kituo cha kawe eneo la mapokezi na kusima nyuma yao.
Mtangazaji akaendelea kusimulia stori ya kibaka mwizi sugu.
Ndipo wale raia wema ilibidi wasimame gafla kwa kutoamini nini kilichotokea hadi mwizi kukimbilia upande wa kituo cha polisi.
Wale raia wema wakashauliana mmojawapo aende kuchukua yule mwizi sugu toka mikononi mwa polisi.
Ndipo njemba mmoja alichomoka na kuelekea alipo mwizi sugu katika kituo cha polisi.
Alipofika katika eneo ambapo yule mwizi mwizi chini ya ulinzi wa askari polisi
Askari polisi wakamuliza yule raia mwema? Una shida gani kijana!
Naye akamjibu, nimekuja kuchukua ndugu yangu huyo hapo
Huyu ndugu yetu ana matatizo ya akili siku nyingi.
Kwa sauti kubwa yule mwizi akajibu, Muongo Muongo mimi ni mwizi na wanataka kuniua.
Wakati polisi wakiwa katika mshangao kwa yote yanayotokea
Mara yule raia mwema akawa anajeuka upande mwingine ili kurudi nyuma gafla chuma kizito kikaanguka kutoka mfukoni mwake.
Basi yule mwizi akasema unaona askari chuma alichobeba anataka kuniua huyu.
Kumbe yule mwizi naye anajua kazi ya askari ni kuleta amani pale palipo na machafuko.
Kazi ya askari kusikiliza pande zote mbili zenye malalamiko ili kufanya uchunguzi na kujua nani ni mkosaji.
Askari alichofanya ni kuwakamata wote wawili na kuwakilisha chini mapokezi kwa muda.
Najua unanishanga Kwanini wote wawili na si akamatwe yule mwizi sugu.
Wakati huyu ni mwizi na amekuwa akifanya wizi leo na siku zote za ujana wake.
Yule askari akaja na karatasi za kuandika ripoti ya kesi iliyopo mbele yake.
Wa kwanza kuitwa kutoa maelezo yake ni yule mwizi sugu kwa yeye ndiye wa kwanza kufika kituo cha polisi.
Askari akaanza.. Unaitwa nani ndugu yangu.
Mwizi akajibu.. Naitwa... .
Una miaka mingapi!
Mwizi akajibu kumi na saba!√
Unaishi wapi
Mwizi akajibu kivukoni!
Kwanini umekuja hapa katika kituo cha polisi!
Mwizi.. Kimya
Askari akamgeukia tena yule mwizi sugu na swali lile lile.
Mwizi Sugu Kimya tena..
Basi askari polisi akumweleza kama huna jibu basi nitakukabizi kwa ndugu yako.
Yule mwizi sugu akajibu
Wataniua Watamuua.. Huyu siyo ndugu yangu kwanza simjui huyu huku akilia
Ndipo yule askari polisi akamuuliza swali lile mara ya tatu
Mwizi akajibu
Yeye ni mwizi na kazi zake mchana ni
mpiga debe wa daladala na usiku wanajikusanya na kuiba katika nyumba za watu au vifaa katika magari.
Askari akamwambia weka sahihi yako katika maelezo haya.
Mwizi sugu akachukua peni na kumwaga wino au sahihi katika maelezo yake.
Askari akamchukua na kumweka ndani mpaka siku inayofuata.
Jaribu kuwaza askari polisi alifanya maamuzi gani kwa yule raia mwema.
Mwisho
Kennedy Kimaro
@kennedytz2
Posted by Kennedytz at 7/21/2017 08:35:00 PM
Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;
si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;
ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Hayo ni mazuri, tena yana faida kwa wanadamu.
Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.
Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae;
ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.
Posted by Kennedytz at 7/11/2017 09:17:00 PM
Today 1/10/ ★ ------- ★
Today I’ve grown exactly ---years old.
Hello mbezisokoni,Kennedy Kimaro
We at JamiiForums The Home of Great Thinkers would like to wish you a happy birthday today!
Subi has left a new comment.":
Happy Birthday to you Kennedy!
Hongera sana kwa kuadhimisha sikukuu yako ya kuzaliwa.
Mungu akujaalie neema, baraka na mafanikio tele katika siku za uhai wako!
Kaka.
The press
Television
Radio
News agency
© Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO
Rudi TOP-Juu